IJA yatoa mafunzo kwa Makatibu Muhtasi wa Mahakama Tanzania
                        
                    
                
            
                            IJA yatoa mafunzo kwa Makatibu Muhtasi wa Mahakama Tanzania
                        
                    
                        
                             Imewekwa: 10 September, 2024
                        
                    
                
                    Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo, Jaji wa Mahakama ya Rufaa na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto leo tarehe 9 Agosti, 2022 amefungua mafunzo ya siku tano kwa Makatibu Mahsusi wapatao 56 wa Mahakama ya Tanzania yanayohusu Namna Bora ya Uendeshaji wa Ofisi. Mafunzo hayo yanayofanyika kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 09 Agosti ,2022 mpaka 13 Agosti, 2022 katika ukumbi wa Mafunzo uliopo Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.