(IJA)

CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA

LUSHOTO

  1. Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kinapenda kuutangazia umma kwamba kinatarajia kufanya mafunzo yanayowalenga wale wote wenye nia ya kuomba na kufanya kazi ya Udalali wa Mahakama na Usambaza Nyaraka za Mahakama kwa mujibu wa Kanuni za Madalali wa Mahakama na Wasambaza Nyaraka za Mahakama, Tangazo la Serikali Namba 363 la 2017 (The Court Brokers and Process Servers (Appointment, Remuneration and Disciplinary) Rules, GN. No. 363 of 2017).
  2. Muda na Mahali: Mafunzo hayo yatafanyika kuanzia tarehe 10 Juni 2019 hadi tarehe 23 Juni 2019 katika Taasisi ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) jijini Dar es Salaam.
  3. Sifa za Waombaji: Muombaji anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:- a) Awe raia na Mkazi wa Tanzania mwenye umri wa utu uzima. b) Awe na Elimu ya kidato cha Nne na kuendelea na awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza Kingereza na Kiswahili kwa ufasaha. c) Awe ni mtu mwenye tabia njema na muadilifu wa kiwango cha hali ya juu na ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa makosa ya jinai/yahusuyo kukosa uaminifu au uadilifu.
  4. Ada ya ushiriki: Kwa washiriki wa mafunzo ya Udalali wa Mahakama, ada itakuwa ni shilingi 970,000/=. Kwa washiriki wa mafunzo ya Wasambaza Nyaraka za Mahakama, ada itakuwa ni shilingi 650,000/=
  5. Jinsi ya kutuma maombi: Waombaji wanaweza kuingia katika tovuti ya Chuo www.ija.ac.tz ili kupata fomu ya maombi kisha kuijaza na kuiwasilisha chuoni kwa njia ya posta (E.M.S.) au kwa anuani ya barua pepe iliyopo kwenye fomu ya maombi ama kufika chuoni na kuiwasilisha kwenye ofisi ya Mkuu wa Chuo.
  6. Fomu ya maombi iambatanishwe, a) Kivuli cha Cheti cha Elimu ya Kidato cha Nne na kuendelea. b) Kivuli cha Cheti cha kuzaliwa au kitambulisho cha uraia. c) Nakala ya risiti ya malipo ya ada ya maombi ya Shilingi 30,000/=. Bofya hapa kuipata Fomu ya maombi http://www.ija.ac.tz/uploads/publications/en155514...
  7. Malipo yote yafanyike kwenye akaunti ifuatayo: Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, NMB A/C, No. 416011100043.
  8. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya Chuo www.ija.ac.tz au piga simu zifuatazo:- +255-27-2660133 au 0784 893676 au 0658 154242.
  9. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 7/05/2019.
Imetolewa na:

Mkuu wa Chuo,

Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA),

S.L.P.20

Lushoto.