(IJA)

CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA

LUSHOTO

TANGAZO KWA UMMA

MAFUNZO YA MADALALI NA WASAMBAZA WITO WA MAHAKAMA

1.Kwa mujibu wa Kanuni ya 6 (e) ya Kanuni za Madalali wa Mahakama na Wasambaza Nyaraka za Mahakama Na. 363 za Mwaka 2017 (The Court Brokers and Process Servers (Appointment Remuneration and Discipline) Rules, GN No. 363 of 2017), Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania, wanautaarifu umma kwamba wanatarajia kuendesha mafunzo maalumu kwa madalali na wasambaza wito wa Mahakama. Mafunzo haya yanalenga watu wnaotarajia kuomba kazi ya Udalali na Usambazaji wito wa Mahakama.

2.Muda na Mahali: Mafunzo hayo yatafanyika mwanzoni mwa mwaka 2019 katika Ukumbi wa Mafunzo na Habari za Kimahakama uliopo ndani ya eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

3.Sifa za washiriki: Mtu anayependa kushiriki ni lazima awe na sifa zifuatazo:

Awe raia wa Tanzania

Awe na Elimu ya Kidato cha Nne na kuendelea na awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza Kingereza na Kiswahili kwa ufasaha

Awe ni mtu mwenye tabia njema na muadilifu wa kiwango cha hali ya juu na ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa makosa ya jinai/yahusuyo kukosa uaminifu au uadirifu.

4.Ada ya kushiriki: Kwa washiriki wa mafunzo ya udalali wa Mahakama, ada itakuwa ni Shilingi 970,000/-. Kwa washiriki wa mafunzo ya wasambaza wito, ada itakuwa ni Shilingi 650,000/-

5.Maombi yaambatanishwe na:-

Kivuli cha Cheti cha Elimu ya Kidato cha Nne na kuendelea.

Kivuli cha cheti cha kuzaliwa au kitambulisho cha uraia.

6.Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15/02/2019. Mwombaji atume maombi yake kwa njia ya Posta (E.M.S), barua pepe au kwa mkono katika anwani ifuatayo:-

Mkuu wa chuo,

Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA),

S. L. P. 20,

LUSHOTO – TANGA.

Barua pepe info@ija.ac.tz.

7.Kwa maelezo au/na ufafanuzi zaidi tafadhali wasiliana nasi kupitia namba za simu zifuatazo: +255-27-2660133 au 0784-920045.

Imetolewa na:

Mkuu wa chuo,

Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA),

Lushoto, Tanga.