MAFUNZO YA MADALALI NA WASAMBAZAJI WITO WA MAHAKAMA
Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania, wanauarifu umma na madalali wote wa Mahakama kuwa wanatarajia kuendesha mafunzo maalum kwa madalali na wasambazaji wito wa Mahakama yatakayofanyika katika ukumbi wa Mafunzo na Habari za Kimahakama uliopo ndani ya eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salam.
Mafunzo hayo yataendeshwa kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ni kuanzia tarehe 02 hadi 06 Julai 2018 ambayo itahusisha Madalali ambao leseni zao za udalali wa Mahakama zimefika ukomo.
Awamu ya pili itahusisha waombaji wapya na itaendeshwa kuanzia tarehe 30 Julai 2018 hadi tarehe 10 Agosti 2018. Anayependa kushiriki ni lazima awe na sifa zifuatazo:
Awe raia wa Tanzania aliye hitimu Kidato cha Nne na kuendelea.
Mahali: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu – Dar es Salaam – Ukumbi wa Mafunzo na Habari za Kimahakama.
Ada: Shilingi 970,000/= Kwa washiriki wa mafunzo ya udalali wa Mahakama na Shilingi 650,000/= kwa washiriki wa mafunzo ya wasambazaji wito.
Malipo yafanyike kupitia akaunti ya chuo – Institute of Judicial Administration Lushoto (IJA) akaunti namba 41601100043 NMB – Lushoto.
Uthibitisho wa malipo na ushiriki ufanywe kwa njia ya barua pepe: info@ija.ac.tz. Kwa mawasiliano zaidi, tafadhali wasiliana nasi kupitia namba zifuatazo: +255 – 27 2660133 au 0655 – 842440
Mkuu wa Chuo
Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA)
Lushoto, Tanga