Posts by admin

Ujumbe wa Benki ya Dunia Watembelea IJA

Leo tarehe 24 Februari, 2024 ujumbe wa Benki ya Dunia umetembelea mradi wa ujenzi wa studio ya jukwaa la kufundishia kwa njia ya mtandao ‘e-learning’ unaofanyika katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. Mradi huo ni kati ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na Mahakama ya Tanzania kwa ufadhili wa Benki wa Benki ya Dunia.
Ziara hiyo imewakilishwa na Maafisa wanne kutoka Benki ya Dunia ukiwa unaongozwa na Bi. Christine Owuor na Maafisa wengine watatu. Pamoja na Maafisa hao pia kulikuwa na watumishi kadhaa wa Mahakama ya Tanzania akiwemo Jaji Mahakama Kuu ya Tanzania ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Maboresho, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Dkt. Angelo Rumisha.
Baada ya kuwasili Chuoni ujumbe huo ulifika katika eneo la Mradi wa ujenzi wa Studio jukwaa la kufundishia kwa njia ya mtandao ‘e-learning’ ambao umeanza tarehe 18 Februari, 2024 na unategemea kumalizika tarehe 18 Mei.
Ujumbe huo pia ulipata maelezo ya uundwaji na matumizi ya studio hiyo itakavyo fanya kazi kutoka kwa Mhandishi Emmanuel Mbosso wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo. Pia alieleza kwa ugeni kuwa Jukwaa la kujifunzia mtandaoni limetengenezwa na wataalamu wa ndani ya Tanzania ambao ni kutoka Mahakama ya Tanzania, Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Chuo cha Serikali za Mitaa (Hombolo).
Jukwaa la mafunzo ya mtandao litarahisisha utoaji wa mafunzo kwa watumishi wengi wa mahakama, kwa gharama nafuu na kupunguza umbali wa kufuata mafunzo.

Read more